WASIMAMIZI WASAIDI MANISPAA YA SINGIDA WAPIGWA MSASA

 

Na Amini Nyaungo

 


Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wametakiwa kufuata katiba na utaratibu ili uchaguzi ufanyike kwa haki na weledi wa hali ya juu.

 


Hayo ameyasema leo Msimamizi wa Uchaguzi  Jimbo la Singida Mjini Aminiel Mfinanga alipokuwa mgeni rasmi katika ufugnuzi wa mafunzo ya siku tatu ya wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Kata katika Manispaa ya Singida.

 


“ Najua mafunzo haya yatawaweka vizuri kuwakumbusha utaratibu wa uchaguzi , ili uchaguzi uwe mzuri lazima mtende haki kwa washiriki wa vyama vyote,”Mfinanga

 


Katika hatua nyingine amesema kuwa uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na tarabu za katiba na sheria ambazo zinatakiwa kufuatwa, amewataka kuondoa malalamiko na vurugu wakati wote wa uchaguzi.

 


Aidha kwa upande wa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Utemini Mkoani Singida Ferdinandi Njau amewashauri wanaopata mafunzo kufuata sheria.



 


“Katika mambo ya kuzingatia walichoapa wanakizingatia ili uchaguzi uwe huru na haki,” Njau

 

 


Lakini pia Afisa uchaguzi jimbo la Singida Mjini Beno Magessa amesema namna semina hiyo itawasaidia kuwakumbusha maswala ya uchaguzi ambapo kutakuwa na mada 11 zitakazo jadiliwa.

 


“ Jumla ya mada 11 zitajadiliwa kwa siku tatu tunatemea baada ya hapa watakuwa wameelewa na tunategemea uchaguzi utakuwa wa haki na huru,”BENO

 


Kwa upande wa wasimamizi Wasaidizi nao wamesema kuwa mafunzo hayo yatawanufisha katika kutenda haki.

 

 

Mwisho 

Post a Comment

Previous Post Next Post