Na Amini Nyaungo
Wajumbe wa Jimbo la
Iramba Mashariki wameamua kumchagua aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa
Singida mzaliwa wa Mkalama kata ya Nduguti Jesca David Kishoa baada ya
kumpitisha katika kura za maoni kwa kura za kishindo siku ya jana August 04,2025
kwa kumpa kura 5946.
Hii ni baada ya
kurudishwa majina saba (7) ya wagombea ambao walijinadi kwa sera zao na
hatimaye Kishoa kuibuka mshindi kati ya hao.
Kishoa amemshinda aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo hilo Francis Isack aliyepata kura kura 2932 za wajumbe ambazo hazikutosha
kumrudisha katika kinyang’anyiro.
Kupata kura za ndio kwa
Kishoa kuna ashiria yale mazuri aliyoyafanya wakati akiwa Mbunge wa Viti Maalum
kwa kuwa karibu na wananchi pamoja na kuwasikiliza katika adha zao za kawaida
zikijumuisha zile za binafsi pamoja na za ujumla.
Baada ya ushindi huo
Kinachosalia sasa ni kurudishwa jina lake CCM Taifa baada ya mchakato basi sasa
apeperushe bendera ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika Jimbo hilo.
Wengine waliotia nia ni
pamoja na Amani Mwendoss aliyepata kura 76, Amam Kwale kura 216, Ally Hassan
Ilanga kura 526, Allan Joseph Kiula kura 446 na Joel Kingu Misholi kura 316.
Mwisho.




Post a Comment