Na Amini Nyaungo
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania imejaliwa
maliasili ambazo zinaweza kuwa chachu ya maendeleo ya nchi zikiendelea kutumika
vizuri.
Ameyasema hayo leo Julai
18,2025 katika uzinduzi wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025-2050 mkoani
Dodoma.
Katika Hotuba yake Rais
Dokta Samia ameweka wazi kuwa dira imekusudia mambo mengi sana moja wapo ni
kutumia rasilimali za nchi ili kuweka kujiendeleza kiuchumi na KUJITEGEMEA.
Rais Dokta Samia amesema
kuwa Misaada na mikopo ikitumika vizuri inaweza kusaidia maendeleo ya nchi lakini
kipaumbele namba moja katika dira ambayo ameizindua leo ni kutumia rasilimali zilizopo na kujitegemea.
“Misaada na mikopo
ikitumika vizuri inaweza kusaidia maendeleo ya nchi kipaumbele chetu ni kutumia
rasilimali zetu zilizopo ili kuendeleza
nchi yetu kwa hiyo lengo kuu ni kujitegemea,” Rais Dokta Samia.
“Lazima Tanzania iwe
sehemu ya kutumia mabadiliko ya akili mnemba kwendana na dunia ya leo”
Aidha katika hotuba yake
pia ameweza kugusia kuwa ili dira iweze kutumika kama ilivyokusudiwa lazima
Watanzania wote wawe wamoja kulikweka taifa katika maendeleo, akisema
kuwa Serikali,Sekta Binafsi wafanyekazi zaidi kuliko maneno.
“Tumejiwekea lengo la
kuweka taifa Jumuishi lenye haki na maendeleo, katika dira ya 2050 tutende sana
kuliko kusema, Serikali, Sekta binafsi tutende zaidi kuliko kusema,”amesema
Katika sehemu ambazo pia
Rais Dokta Samia amegusia ni pamoja na kutokana na kukua kiuchumi na kuibuka
kwa mataifa mbalimbali kukua kiuchumi taifa la Tanzania katika sera na
diplomasia ya kimataifa itaendelea na sera yake ya kutofungamana nan chi yoyote.
“Tanzania kuendelea na
sera yake ya kutofungamana na nchi yoyote,”
Aidha pia ameelekeza tume
ya taifa ya Mipango waandae haraka nyenzo zitakazo tumika kupima kipimo cha
maendeleo serikalini.
“ Naelekeza kila wizara
kupitia sera zake zile ambazo haziendani na dira hii basi waziache, Tume ya
kurekebisha sharia Tanzania waanze mchakato wa kuchambua juu ya dira hiyo,Kuelekeza
dira ya mipango kuweka mfumo wa muda wa utekelezaji wa hatua kwa hatua, Sekta
binafsi inatakiwa kujipanga ili itekeleze malengo na shabaha ya dira hiyo,”
ameongeza
Mwisho




Post a Comment