Na Robert Onesmo
Makamu Mwenyekiti wa umoja wa vijana(UVCCM) taifa Rehema Omary Sombi ,amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge wa viti maalumu katika uwakilishi wa kundi la vijana taifa
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kurejesha fomu hiyo Rehema, amesema anaipongeza sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi kupitia kwa katibu mkuu wake Dkt .Emmanuel Nchimbi kwa namna alivyoratibu zoezi hili ambalo limeenda kwa amani na utulivu
Kwa upande wake Sombi amejitanabaisha kuwa ameshakwisha kuiva katika eneo la utekelezaji wa irani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
"Niwahakikishie heshima ambayo niliipata nimeshakwisha kukwiva lakini sisi kama chama cha Mapinduzi ni wamiliki wa duka sasa tunaenda kule ili tukatunge sheria ambazo zitawalinda vijana ambapo sisi ndio tunaomba dhamana kwa upande huo"amesema Sombi.
Post a Comment