Na Mwandishi Wetu
Miradi yenye thamani ya zaidi ya Sh.Bilioni 62.6 iliyojengwa katika halmashauri saba zilizopo katika Mkoa wa Singida itazinduliwa na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru 2025 ambao utakimbizwa kwa siku saba mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, ametoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu, Ismail Ally Ussi, baada ya kuupokea katika kijiji cha Sagara Halmashauri ya Wilaya ya Sibgida ukitokea Mkoa wa Manyara.
Amesema katika miradi hiyo mchango wa serikali kuu ni asilimia 92,asilimia 6.7 wahisani, halmashauri asilimia 1 na wananchi ni asilimia 0.2.
Dendego amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Mkoa wa Singida utakimbizwa jumla ya kilometa 842.6 katika halmashauri zote saba za mkoa huu na kwamba kila eneo wananchi wamejipanga kuupokea.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi Mkuu unaitarajia kufanyika Oktoba mwaka huu alisema mkoa umejipanga vizuri ambapo asilimia 99.6 ya wananchi wa Singida wamejiandikisha kwa ajili ya kushiriki uchaguzi huo.
Mwisho

Post a Comment