JOANFAITH AINGIA KATIKA KITABU BORA CHA WAKURUGENZI SINGIDA


Na Amini Nyaungo


Waswahili husema kila chenye thamani aijuaye mwenye chake ndipo ambapo Wananchi wa Mkoa wa Singida wanavyowapenda viongozi wao ukiongozwa na Halima Dendego kwa upande wa serikali huku katika chama ikiongozwa na Martha Mlata.

Leo tutaangazia zaidi Halmashauri ya Manispaa ya Singida ambapo zamani ili fahamika kama Mji wa Singida.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida Joanfaith Kataraia ameingia katika orodha ya Wakurugenzi waliowahi kuhudumu katika Mkoa wa Singida.

Kataraia ni Mkurugenzi wa 15 katika wote waliowahi kuhudumu ndani ya Manispaa ya Singida akiendelea kuhudumu vizuri na kwa moyo wake wote.

Ikumbukwe kabla ya kuwa Manispaa ya Singida zamani ilikuwa inaitwa MJI WA SINGIDA ambapo hawa Wakurugenzi waliitwa Mkurugenzi wa Mji wa Singida.



Na Joanfaith yeye anashika namba 15 ukiwajumlisha wote lakini tangu iitwe Manispaa ya Singida anashika namba 9 baada ya Jeshi Lupembe.

Orodha yao unaipata pamoja na miaka yao waliyowahi kuhudumu katika Wilaya hii ya Singida kupitia Makala hii.

Aliyeanzisha dimba baada ya miaka 17 kupita tangu uanzishwe Mkoa wa Singida ni Juma A. Lupendelle yeye ameshika nafasi ya kwanza amehudumu kwa muda wa miaka 5 kisha akapata uhamisho, mzee wetu huyu alianzia mwaka 1980 hadi 1985.

Maana Mkoa wa Singida umeanzishwa Oktoka 15,1963 hadi sasa una miaka 65 tangu kuanzishwa kwake.

Baada ya hapo namba mbili ameishika ndugu Ndeshukurwa A. Sumari yeye amecheza vyema kwa miaka mine 1985 hadi 1989 akiitumikia Singida.

Orodha yetu inaendelea namba tatu ni Abubakari D.O. Midello yeye ameongoza kuanzia mwaka 1989 hadi 1991 kwa miaka mitatu.

Bwana Shaibu Z. Muyinga ameiongoza Halmashauri kwa miaka 3 akianzia mwaka 1991 hadi mwaka 1994 ndipo akaachia kombe liende kwa Davis H. A. Njau aliyeongoza kwa mwaka mmoja kutokea 1995 hadi 1996.

Aliyevunja rekodi ni Sabini I. Sirima yeye ameongoza kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2004 kwa miaka 8 akiwa ndani ya Singida.

Ndipo akaichukua Bernadette Kinabo (MS) hapa sasa imebadilika kuwa Manispaa akaichukua na kuongoza kwa miaka 2 kuanzia 2004 hadi 2006.

Bwana Robert Matondo Kitimbo yeye ameanzia mwaka 2006 hadi 2009 ikiwa wote wana lengo moja la kuleta maendeleo.

Safari imeendelea ambapo Yona L. Maki ameichukua Manispaa ya Singida kuanzia mwkaa 2009 hadi 20212.

Mathias E. Mwangu amehudumu kwa mwaka mmoja ameanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2013 akaichukua Joespeh S. Mchina amehudumu kuanzia mwaka 2013 hadi 2016 Manispaa ikaenda kwa Bravo K. Lyapembile .



Ndugu Zerin K. Lubuva naye amepata kuhudumia Manispaa hii kuanzia mwaka 2021 hadi 2022 kila mmoja amehudumu kwa moyo na umahiri sana.



Mwaka 2023 hadi mwaka 2024 Jeshi G. Lupembe naye amechukua Manispaa ya Singida ameongoza kwa mwaka mmoja alijitahdi kadri alivyo jaaliwa na kombe likaenda kwa Joanfaith Kataraia.

Sasa kombe lipo kwa mwanadada mahiri mrembo dada yetu wa Manispaa Joanfaith Kataria ndio anaishikilia hadi sasa Na bahati nzuri kwa sasa mbio za Mwenge wa Uhuru zinaendelea ikiwa katika Halmashauri yake amefanya vizuri sana.

Kataria ni mwanadada anayewakilisha vizuri viongozi wa kike wa mkoa wa Singida.

Kataraia alifanya vyema sana alipokuwa Morogoro na Mheshimiwa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan akamuona anafaa aje mkoa wa Singida. 

Chamber Talk Show leo ndio inakularibisha rasmi uendelee kupiga kazi na Manispaa ya Singida itaandikwa jina lako.

Mwisho.


Post a Comment

Previous Post Next Post