AHUKUMIWA JELA MIAKA 3 AU KULIPA MILIONI 5 KWA KOSA LA KUTOA TAARIFA ZA UONGO



 Na Sylvester Richard



Zuberi Saidi Nkoko ( 59 ) Mkazi wa Misuna, Manispaa ya Singida amehukumiwa kwenda jela miaka 3 au kulipa faini ya shilingi za kitanzania ( Tsh.) milioni 5 pamoja na simu yake ya mkononi kutaifishwa kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kinyume cha sheria. 


Mshtakiwa alitenda kosa hilo Juni 02, 2025 katika maeneo ya Misuna, Kata ya Misuna, Wilaya na Mkoa wa Singida ambapo alitoa taarifa ya uongo yenye taswira ya kulichafua Jeshi la Polisi Tanzania hivyo kukamatwa na Jeshi la Polisi kisha kufikishwa mahakamani Juni 19, 2025. 



Aidha, Mahakama imetoa hukumu hiyo Julai 04, 2025 mbele ya Mhe. Fadhili Luvinga ambaye ni Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Singida na mshitakiwa ametumikia adhabu hiyo kwa kulipa faini kama Mahakama ilivyomwadhibu.

Post a Comment

Previous Post Next Post