MKALAMA WADHAMIRIA MAPINDUZI SEKTA YAKILIMO

Na Amini Nyaungo



Kilimo kimeendeleza kuwa nguzo muhimu ya uchumi kwa wananchi wa Mkalama katika uzalishaji wa mazao ya chakula ambapo umeongezeka kutoka tani 116,948 katika msimu wa 2024/2025 hadi tani 354,438 katika msimu wa 2025/2026.


Hayo ameeleza leo Julai 01,2026 Mkurugenzi Halmashauri ya Mkalama Asia Messos alipoongea na Waandishi wa Habari  kuhusu miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo.



Asia amesema kuwa mazao ya biashara na uzalishaji umeongezeka kutoka 44,796 hadi tani 50,471 kwa kipindi hicho.


Mafanikio haya yamechagizwa kuongezeka kwa maafisa ugani kutoka 16 hadi 47 lakini pia imechagizwa na matumizi ya mbegu bora na mbolea kupitia ruzuku ya Serikali.



 Jumla pembejeo za ruzuku zenye thamani ya shilingi 9,488,500,00 zimesambazwa kwa wananchi pamoja na utekelezaju wa mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umeimarisha masoko pamoja na utekelezaji jumla sh 8,143,989.09 zililipwa kwa wakulima kupitia mfumo huu na shiling 246,688,529 kwa ajili ya ushuru wa Dengu.


Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post