RAIS DKT. SAMIA AMEITENDEA HAKI MIRADI YOTE ILIYOANZISHWA NA MTANGULIZI WAKE- JAPHARI

  

 

Na Amini Nyaungo



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. Samia Suluhu Hassani ameitendea haki miradi yote iliyoanzishwa na mtangulizi wake hayati DKT John Joseph Magufuli hivyo anastahili  kuwa katika kiti hicho kwa awamu nyingine ili amalize yale yaliyobaki.



Hayo ameyasema leo Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Japhari Saidi alipoongea na Waandishi wa Habari leo (Juni 8,2025) katika ukumbi wa Rafiki Mkoani hapa.



Aidha katika mkutano huo ameweka wazi kuwa pasipo na mashaka Rais DKT. Samia ameendeleza pale ambapo mtangulizi wake amepaachaa kwani ameweza kuitendea haki miradi mikubwa ya maendeleo.

“ Rais DKT. Samia ameitendea haki miradi yote iliyoanzishwa na mtangulizi wake,” amesema

Japhari ameweka bayana kuwa anayoyafanya hivi sasa  Rais Dokta Samia Suluhu Hassan ni kielelezo cha ukomavu na uzalendo katika aifa hili la Tanzania.

“Anayoyafanya Rais DKt Samia ni kielelezo cha ukomavu na uzalendo wake kwa Taifa la Tanzania,” Japhari



Kada huyo ameenda mbali Zaidi na kusema kuwa kwa yote aliyoyafanya anastahili kuwa katika nafasi aliyyopo hivi sasa kwani ameimudu vizuri.

“ Rais DKt Samia amethibitisha pasipo shaka yeyote kuwa anatosha kwa nafasi hiyo,” Ameongeza

Licha ya hayo amesema kuwa kila idara hivi sasa iko katika wakati mzuri kwani katika uongozi wake ameweza kuimarisha utu na usawa kuanzia katika afya, michezo hadi Sanaa huku akiwa kinara katika kuweka sawa miundombinu.



“Kwa wakati huu kila kitu kipo vizuri ukiangalia katika michezo viwanja vizuri vipo kwa ajili ya kuchezo michuano mikubwa ya kimataifa na kitaifa kwenye afya nako amefanya vizuri kwani kuna zahanati kila sehemu pamoja na miundombinu bora,”

Mwisho 

Post a Comment

Previous Post Next Post