Na Amini Nyaungo
Msanii wa kizazi kipya mwenye maneno mengi ya kuvutia Mbosso amefanikiwa kupokelewa vizuri baada ya kutoka katika 'Label' ya Diamond Platnumz.
Baada ya kutoka alikaa kidogo kwa ajili ya kupika muziki mzuri kwa ajili ya mashabiki wake na hatimaye watu wamempokea vyema akirudi kivingine akijisimamia mwenyewe.
Mbosso ametoa 'Extended Playlist' (EP) yenye vibao saba huku 'Pawa' ndio ambayo inabamba zaidi katika EP hiyo vibao vingine ni pamoja na 'Asumani, Aviola, Tena, Siko Single, Merija, Nusu saa pamoja na Pawa.
Pawa ina watazamaji zaidi ya milioni mbili ikiwa katika mtandao wa youtube akifanya vizuri na umekuwa midomoni mwa mashabiki wake.
Kwa namna hiyo Mbosso amefanikiwa na sasa anaouwezo wa kwenda mbele zaidu kama ambaylvyo ilivyokuwa zamani, ataweza kufanyakazi nzuri zaidi baada ya mapokeo haya.
Hii inafanana na ile ya Harmonize aliewahi kutoka katika 'Label' hiyo na kupokelewa vizuri yeye akatoka na ngoma inayoitwa 'Uno'
Mbosso alitoka katika 'Label' japo haijafahamika nini kimefanya atoke katika 'Label' hiyo.
Mbosso aliwahikutamba na band ya 'Yamoto Band' ambayo imemtoa akiwa na wasanii wengine kama vile Aslay, Beka Flava, Ebock Bella pamoja na Mbosso.
Lakini pia ametamba katika vibao kamanvile 'Tamba, Huyu hapa na vingine vingi vikali.
Mwisho.




Post a Comment