Na Mussa Mkilanya
Jumla ya wahitimu 220 wa taaluma ya habari kutoka katika chuo cha uandishi wa habari Rida kilichopo Tabata Segerea wamefanya mahafali ya kuhitimu taaluma ya habari katika ngazi mbalimbali.Akizungumza katika ukumbi wa Blessing Tabata Segerea jana April 30 mwaka huu, wakati akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa chuo hicho madame Angel Adolf amesema Rida institute leo kimefanya mahafali ya tatu katika kipindi cha miaka kumi na moja tangu chuo hicho kuanzishwa.
Madame Angel, ameongeza kuwa chuo cha Rida kimepata mafanikio mbalimbali katika kipindi hicho ikiwemo kumiliki eneo lake, kutoa wanafunzi wengi wa fani ya habari katika ngazi mbalimbali ambao wanafanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Kwa upande wake mgeni rasmi Augustino Godfrey amesema, taaluma ya habari ni taaluma muhimu sana nchini na duniani hivyo amesisitiza wahitimu kutumia taaluma hiyo kwa uzalendo na ustawi wa Taifa.
Nae mwenyekiti wa Bodi ya chuo hicho Alfonce Ngalafai katika risala yake amewaasa wahitimu hao kutumia taaluma yame yahari kuchochea maendeleo na kueleimisha jamii.
Aidha ameongeza kuwa ni vyema mwandishi akawa na malengo chanya na taaluma yake badala ya kukubali kulaghaiwa na watu wache wenye nia ovu na kutumika kusababisha machafuko au taharuki zingine jambo ambalo litakuwa nikinyume na maadili ya taaluma ya habari.
Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wamesema wamepokea nasaha za viongozi hao na kwamba wataitumia taaluma hiyo vyema kwa manufaa ya Taifa na kwamba watakuwa mabalozi wazuri wa chuo hicho.
Mwisho



Post a Comment