Na Mwandishi Wetu, Singida
Mabingwa watetezi wa mchezo wa mpira wa miguu katika michuano ya Kombe la Mei Mosi timu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamezinduka na kuwafunga bila huruma Tume ya Maendeleo ya Jamii kwa magoli 9-1 katika mchezo wa robo fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Airtel mkoani Singida.TANESCO awali ilianza kwa kusuasua kwenye mechi ya makundi ambapo ilimaliza ikiw ana pointi tisa sawa na Wizar aya Maliasili sasa imeonesha matumaini ya kutetea ubingwa wake walioupata mwaka 2024 mkoani Arusha.
Katika mchezo mwingine uliokuwa na ushindani mkubwa uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Liti timu ya Wizara ya Fedha waliwafunga Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mabao 2-1.Tayari TANESCO na Wizara ya Fedha wametangulia kuingia hatua ya nusu fainali kwa mchezo wa mpira wa miguu na wanawasubiri kati ya Wizara za Mamboi ya Ndani dhidi ya Wizara ya Maliasili na Utalii; na Wizara ya Mambo ya Nje dhidi ya Wizara ya Afya.
Katika mchezo wa kuvutana kwa kamba timu zilizochuana kwenye hatiua ya trobo fainali iliyofanyika kwenye uwanja wa Magereza, ambapo timu ya wanaume ya Ofisi ya Rais Ikulu waliwavuta Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) kwa mvuto 1-0; huku Wizara ya Uchukuzi wamewavuta Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) kwa mivuto 2-0; nayo Wizara ya Maliasili na Utalii waliwavuta Wizara ya Fedha kwa 2-0 na Wizara ya Mambo ya Ndani waliwashinda Wizara ya Fedha kwa 2-0.
Kwa upande wanawake Wizara ya Mambo ya Ndani waliwashinda Wizara ya Madini kwa 2-0; huku TAKUKURU wakiwavuta Maliasili na Utalii kwa 2-0, nao Wizara ya Uchukuzi wakiwavuta TAMISEMI kwa 2-0 na Wizara ya Afya waliwaadhibu Wizara ya Fedha kwa kuwavuta mivuto 2-0.
Katika hatua nyingine timu ya wanaume ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wametwaa ushindi wa tatu kwa kuwafunga TANESCO kwa pointi 92-58 katika mchezo uliofanyika kwenye shule ya msingi Mwaja.
MWISHO

Post a Comment