Na Amini Nyaungo
Singida moja ya mikoa ambayo
imechangamka katika kila nyanja, upande wa michezo uko sawa, upande wa vyombo
vya habari nayo inafanya vyema katika kuutangaza Mkoa wa Singida kila mmoja anafanya
katika upande wake.
Upande wa siasa pia
unaendelea kufanya vizuri mno Singida imetoa Waziri wa Fedha ambaye ni Mwigulu
Lameck Nchemba ina viongozi wakubwa ambao wanaiwakilisha vyema Singida.
Makala yangu inaangaziaa
zaidi Manispaa ya Singida ambapo ina historia nzuri mno ila leo nitaangalia
historia ndogo sana ya Manispaa hii ilipoanzia hadi kufikia leo na huko mbele
utaona dhamira ya kichwa cha habari hapo juu.
Kabla ya kuwa Manispaa ya
Singida hapo zamani iliitwa Halmashauri ya Mji wa Singida wakati harakati za
kumegwa kati ya Singida Mjini na Singida Vijijini ilipatwa kuitwa Wilaya Ndogo
na miongoni mwa Wakurugenzi wa mwanzoni kabisa walikuwa ndugu Lipendele pamoja
na mama yetu mama Sumari.
Hata hivyo Wilaya ndogo
hiyo haikupewa Mkuu wa Wilaya bali Mkuu wa Wilaya ya Singida aliendelea
kutawala Wilaya zote mbili hali ambayo imeendelea hadi hivi sasa.
Kiini cha Makala hii huko
kote nimekupa historia lengo langu ni kuangazia viongozi ambao waliwahi
kuongoza kuanzia Halmashauri ya Mji wa
Singida hadi kuitwa Manispaa ya Singida na hapa tunaanzia mwaka 1981 katika eneo la uongozi ambapo
zamani waliitwa Wenyeviti wa Mji wa Singida kwa sasa wanaitwa Meya.
Ni miaka 20 sasa imepita
tangu ibadilishwe na kuitwa Manispaa ya Singida na hapo sasa pia imebadilika
viongozi wake waliitwa MEYA yaani Meya wa Manispaa ya Singida.
Tukianzia hapo Yagi
Maulid Kiaratu ambaye sasa anagombania Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini akiongoza katika kura za maoni za wajumbe ila kabla ya hapo alikuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ambapo anakuwa ni
wa tatu baada ya wawili kutangulia kuongoza Manispaa hii( Yaani hao wawili na
ukijumisha Mheshimia Yagi wanakuwa wa tatu
na ukijumlisha na wale wenyeviti wanakuwa 8).
Wameanza kuitwa Meya wa
Manispaa ya Singida mwaka 2005 hadi sasa ni miaka 20 imepita na mji wa Singida
unaendelea kuwa katika mazingira mazuri.
Wakwanza kabisa kuzindua
kuwa Meya wa Manispaa ya Singida ni ndugu yetu Mheshimiwa Salum Mahami yeye
amekaa hapo kwa miaka kumi kuanzia 2005 hadi 2015.
Mwaka 2015 hadi 2020
amechukua mzee wetu Mheshimiwa Gwae C. Mbua
kwa miaka mitano ambayo amehudumu kama Meya wa Manispaa ya Singida.
Wakati huo Gwae anachukua
jukumu la kuwa Meya moja ya wasaidizi wake katika hiyo miaka 5 aliyohudumu Mheshimiwa Yagi Kiaratu aliwahi kuwa Naibu
Meya na kufanyanae kazi vyema sana.
Ngoma imebadilika kutoka
kuwa Naibu Meya ambapo mwaka 2020 hadi 2025 Mheshimiwa Mstahiki Meya Yagi
Kiaratu amekuwa akiongoza kiti hiko kwa uzuri sana na roho safi sana.
Hivi sasa Gwae Mbua ndio
Naibu Mstahiki Meya kibao kimegeuka na historia imeandikwa kwa wino mweusi kwa
kukolezwa.
Yagi amekuwa akifanya
mzuri na kuipendezesha Manispaa ya
Singida na ni mmoja ya viongozi wenye mvuto wa hali ya juu sana.
Mji wa Singida unakua na
unaendelea kupendeza hivi sasa yote haya ni usimamizi mzuri wa viongozi wa mkoa
wa Singida pamojana Mstahiki Meya Yagi Kiaratu.
Kwanini mama huyu
asiandikwe katika wino mweusi na kukolezwa kwa jitihada anazozifanya ? ni jembe
sana huyu mama wala sio masikhara, ana utu na utulivu pamoja na kujali watu
wake.
Pia ni diwani wa kata ya Majengo hebu kaangalie katika Kata
hiyo namna ambavyo imejengeka na ilivyosafi kazi yake imeendelea kuonekana.
Ukiachana na hapo orodha
ya MEYA tangu iiliyobadilika mwaka 2005 ifuatayo ni orodha ya Wenyeviti wa Mji wa Singia rasmi ilianzia
mwaka 1981 ambapo Mathayo J. Hango ameongoza kiti hiki kwa mwaka mmoja mmoja hadi
mwaka 1982.
Safari iliendelea ambapo
Rajabu W. Munkhola amechukua nafasi hiyo mwaka 1983 hadi Disemba 1983 akaachia
ngazi na kuwapa kijiti wengine.
Mwaka 1984 hadi 1988
alikuja ndugu Hassan T. Simba yeye amekaa kwa miaka mine katika cheo hicho
ambacho kwa sasa ndio kama Meya wakati huo kinaitwa Mwenyekiti wa Mji wa
Singida.
Baada ya hapo akachukua
nafasi Hassani Simba Ikuja kutokea mwaka 1989 hadi 1998 yeye amekaa kwa miaka 9
katika kiti hicho na kumuachia mwingine.
Katika orodha hiyo wa
mwisho alikuwa Salum M. Mahami yeye sasa akaongoza kuanzia 1998 hadi mwaka 2005
amekaa kwa miaka 7.
Baada ya hapo ndio
ikabadilika ikawa Manispaa ya Singida ambayo tayari nimeielezea juu kuanzia
mwaka 2005 hadi sasa 2025 inatambulika kama Manispaa ya Singida na wanaoongoza
ni Meya sio Mwenyekiti tena wa mji wa Singida.
Kwa ujumla wake ni
viongozi 8 ambao kila mmoja ametoa huduma yake kwa vile ambavyo Mungu
alivyomjalia na kuiongoza Singida katika njia salama.
Manispaa ya Singida ndio
ina kila kitu ina soko kuu la Mkoa wa
Singida, ina Soko la Vitunguu, ina soko la Matunda ina Stand Kuu ya Mabasi
pamoja na mambo mengine mazuri ambayo yanaipeperusha Singida.
Kwa sasa Mheshimiwa Yagi Kiaratu amepita katika kura za maoni na anasubiri kamati kuu itasemaje juu ya kupeperusha bendela ya Ubunge Jimbo la Singida Mjini.
Yagi kwa Mujibu wa watu mbalimbali anapendwa sana na watu hasa katika kujitoa kwake kwa mtu mmoja mmoja na kundi la watu na Wanasingida kwa ujumla.
Singida ni sehemu salama yoyote aitakaye aje.
Mwisho




Post a Comment