MASTER JAY AKUBALI YAISHE KWA KIBA
Na Amini Nyaungo
Mtayarishaji mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini
Tanzania Joachim Marunda Kimaryo (MASTER JAY) leo aomba kumaliza tofauti yake
na Ali Kiba baada ya kuibuka mjadala ambao alimtuhumu msanii Ali Kiba kuwa
miongoni mwa wabana pua.Master Jay amemuomba radhi Kiba leo katika kipindi cha Jirani kinachorushwa na
Crown Media akisema kuwa hayakuwa maneno mazuri na alitumia kilevi wakati
alipoongea maneno hayo.
Aidha ameweka wazi kuwa alitaka kumfuata Ali Kiba ili
wayamalize na maisha mengine yaendelee kama ilivyokuwa huku akiweka wazi hana
ugomvi wowote na Ali Kiba.
Katika usiku wa fainali ya BSS baada ya kutamatika Master Jay
alihojiwa na chombo kimoja cha habari akisema kuwa Ali Kiba ni mbana pua hawezi
kufananishwa na Bien kutoka Kenya ambaye anaimba muziki wa taratibu wa R&B.MWISHO
Post a Comment