Na Amini Nyaungo
Hayo ameyazungunza leo (March,20,2025)
Mwenyekiti wa Soko Kuu la Vitunguu
mkoani Singida Iddi Mwanja alipozungunza na Chamber Media alipotembelea sokoni
akiwaambia wananchi na wakulima kuwa leo bidhaa imefurika sokoni hivyo
zikiendelea kupakiwa huko mashambani watakosa sehemu ya kushushwa na
kusababisha usumbufu kwa mkulima.
Aidha amejibu juu ya
baadhi ya wafanyabiashara wanaotaka waongeze ujazo ili wanunue Vitunguu hivyo
kwa haraka ameweka bayana kuwa ujazo utabakia kuwa kama ilivyo kawaida gunia
moja ujazo wake ni kilo100 hadi 105 wala hawajazi ‘Shishimbi’ ili kwenda sawa misimamo
waliojiwekea na kama ambavyo serikali inahitaji.
Kwa upande wake Mbuga
Rashidi yeye ni mkulima ameshauri uongozi uongeze ujazo huenda ikawa njia sahihi ili mazao yao yauzwe haraka
“Mie naona waongeze kidogo ujazo ndio inakuwa njia rahisi ya mazao yetu kuuzwa haraka vinginevyo tutakesha hapa,” Mbuga
Akiungwa mkono na Yahya Mohamed ambaye
pia amesema waongeze ujazo ili kila kitu kiende sawa na mzigo uliopo uishe na
wanedelee na shughuli nyingine.
Lakini Omari Shabani yeye amesema
kuwa ni veyma uongozi wawaambie wananchi na wakulima wasilete mazao yao kwanza
hadi mzzigo huu utakapo isha.
“Kwa hapa ili siku ya leo
gunia limesimama hata elfu sabini ambapo juzi tu ilikuwa hadi laki a thelethini
leo mzigo upo wa kutosha hapa hivyo uongozi uone namna ya kuwaambia wakulima
wasilete mazao yao,”
Post a Comment