Na Amini Nyaungo
Tanzania inazidi kusimama na kuendelea kuimarika katika kipindi cha miaka minne ya Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kuwa na hofu ya Mungu katika kuwatumikia wananchi wake katika kuleta maendeleo.Hayo ameyasema leo (March 22,2025)Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Martha Gwau alipokuwa na kina mama wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Wilaya ya Iramba mkoani hapa akisherehekea na kuwaambia wananchi hao kuwa Samia aliyoyafanya yanadhihirika wazi na yanaonekana kwa macho.
"Kwa kipindi hiki cha miaka minne ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassani tunaona wazi machoni mwetu makubwa ambayo ameyafanya katika nchi yetu ya Tanzania, ukitaka shule zinaonekana, Zahanati na Miundombinu vyote vinaonekana kwanini wanawake wenzangu na wananchi wote tusimuunge mkono Rais Samia,"Gwau
Aidha ametumia nafasi hiyo kuwaomba kina mama wa Mkalama kuendele kumuamini na kuyazungunza yote mazuri ambayo ameyafanya kwani Rais Samia ni mtu sahihi ndani ya Chama na Taifa.
Pia amewaomba kina mama hao kuachana na makundi wapendane ili waimarishe umoja na ushindi katika mambo yao mbele ya safari kwani watakuwa na mengi yanayotaka umoja na mshikamano.
Ameweka wazi kuwa pasipo umoja hakuna ushindi wa mtu mmoja mmoja au kikundi hivyo wawe wamoja ili kuleta ushindi ndani yao na chama.
Mwisho





Post a Comment