KUKU KUCHOMWA MEI MOSI SINGIDA, DENDEGO ATHIBITISHA

 Na Charles Kikoricho

Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi duniani maarufu kama mei mosi yanatarajia kufanyika  kitaifa mkoani Singida   Mwaka huu.


Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 11/ 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego wakati akizungumza na kamati  ya maandalizi ya maadhimisho hayo ya  Mkoa na Kitaifa ofisini kwake .


Halima Dendego amesema kuwa shughuli hiyo itafanyika katika uwanja wa liti uliopo Manispaa ya Singida, lakini kabla ya kilele cha siku hiyo ya mei mosi kutakuwa na Shughuli mbalimbali kama vile michezo na jumla ya watu elfu mbili na miatano wanatarajia kushiriki kwenye michezo hiyo.

Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa katika kuendelea kusherehesha shughuli hiyo kutafanyika pia utalii wa Barabarani lengo likiwa kuwaonyesha wageni wataofika Singida wajue Singida kuna utalii gani, lakini pia kutakuwa na Usiku wa Kuku ( kuku festival) Mashindano ya magari, Mashindano na ngumi, maonyesho mbalimbali ya shughuli ambazo wanaSingida wanazifanya, Burudani mbalimbali ikiwemo Ngoma za asili 


Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi TUCTA Tumaini Nyamhokya amesema kuwa kupitia vikao ambavyo wamevifanya kwa kushirikiana na uongozi wa mkuu wa mkoa wa Singida wanamiini sherehe hiyo itafanyika vizuri na itakuwa ni yakipekee

Siku ya Wafanyakazi duniani maarufu kama mei mosi hufanyika kila mwaka lengo likiwa ni kuangalia na kufanya tathimini juu ya haki na usawa kwa wafanyakazi pamoja na usalama wa kazi mahala pakazi..

Post a Comment

Previous Post Next Post