SINGIDA WAKUSANYA ZAIDI YA SHILINGI 15,330,882,122.37 ZA MADUHULI YA SERIKALI

 

Na  Jumbe Ismailly SINGIDA      

 


MKOA wa Singida umefanikiwa kukusanya shilingi 15,330,882,122.37 sawa na asilimia 65.52 ya malengo ya makusanyo ya mwaka ya shilingi 23,400,000,000/= ikiwa ni maduhuli ya serikali yanayotokana na ada mbalimbali za leseni,mrahaba wa madini,ada ya ukaguzi pamoja na tozo zingine.

 

Akizungumzia mafanikio yanayotokana na sekta ya madini katika Mkoa wa Singida,Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Singida,Mhandisi Sabai Nyansiri ameweka bayana kuwa mafanikio hayo yamepatikana katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2024/2025 hadi kufikia mwezi januari,mwaka huu.

 

Akifafanua zaidi afisa huyo wa madini amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2017/2018 Mkoa ulitarajia kukusanya shilingi 1,000,077,979.83 lakini ulikusanya 448,334,958.36 sawa na asilimia 44.83 wakati mwaka 2018/2018 zilikusanywa shilingi 804,522,087.34 sawa na asilimia 80.49 ya lengo la makusanyo ya 1,000,649,362.36.

 

Amesema kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 Mkoa wa Singida ulivuka lengo la makusanyo kwa asilimia 302.31 kwa kukusanya 4,534,666,633.27 kati ya 1,499,988,962.38 wakati mwaka 2020/2021 walikusanya 4,763,652,195.59 sawa na asilimia 158.78 ya lengo la kukusanya 3,000,158,833.35 na mwaka 2021/2022 Mkoa ulifanikiwa kukusanya 6,334,117,171.80 sawa na asilimia 149.04 ya 4,249,944,425.52.

 

Aidha kwa mwaka 2022/2023 Mkoa wa Singida ulikusanya 8,813,945,218.85 sawa na asilimia 88.14 ya 9,999,937,847.56 wakati mwaka 2023/2024 makusanyo yalikuwa 18,951,196,134.79 sawa na asilimia 145.22 ya 13,049,990,452.27 na mwaka 2024/2025 hadi mwezi januari,2025 makusanyo yalikuwa 15,330,882,122.37 sawa na asilimia 65.52 ya lengo la 23,400,000,000/=

 

Akizungumzia makusanyo yaliyopatikana katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000/2001 hadi mwaka 2016/2017 Mhandisi Nyansiri amefafanua kuwa kwa mwaka 2000/2001 Mkoa wa Singida ulikusanya 386,000/=wakati mwaka 2001/2002 2,357,400/= 2002/2003 4,556,066/=,mwaka 2003/2004 4,687,090/=, 2004/2005 16,452,632/= 2005/2006 33,883,300/=, 2006/2007 40,793, 680/=, 2007/2008 38,603,264/= na mwaka 2008/2009  51,944,687.50.

 

Hata hivyo Mhandisi huyo ameweka bayana kuwa mwaka 2009/2010 100,789,623/= mwaka 2010/2011 65,315,425/=, mwaka 2011/2012 169,037,537.50, mwaka 2012/2013  330,696,087.27, mwaka 2013/2014  390,451,565.40, 2014/2015  606,151,565.60, mwaka 2015/2016 673,664,595/= na mwaka 2016/2017  433,653,728.85.

 

Mhandisi Nyansari hata hivyo amezitaja baadhi ya changamoto zinazoikabiliu sekta ya madini kuwa ni pamoja na kuwepo kwa migogoro kati ya wachimbaji wa madini na wamiliki wa ardhi vile vile pia baina ya wachimbaji wadogo wenyewe,miundombinu mibovu ya barabara na ukosefu wa huduma za maji kwa baadhi ya migodi na wachimbaji wadogo na kati kutokuwa na mitaji ya kuendeleza leseni zao.

 

MWISHO.

Post a Comment

Previous Post Next Post