Na Amini Nyaungo
Jamii imehimizwa kujiunga
na mfuko wa Bima ya Afya Taifa (NHIF) ili iwasaidie pale wanapopatwa na
magonjwa mbalimbali watibiwe kwani magonjwa yanakuja bila ya taarifa hivyo
wakiwa na bima wanakuwa tayari kwa ajili ya kupata matibabu.
Hayo ameyasema leo Meneja
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Singida Benjamini Mwalugaja Wilayani
Mkalama ambapo walikuwa wanagawa mifuko hiyo ambayo ndani yake kumesheheni
vifaa kwa ajili ya kina mama kujifungulia yaani ‘’Delivery park’’.
Mwalugaja amesema kuwa
hiyo ni zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya DR.
Irine Isaka kwa ajili ya wanawake
kusaidia kupata vifaa vya kujifungulia akisema kuwa hayo ni maono ya Rais
Daktari Samia Suluhu Hassan katika kutoa huduma bora kwa wananchi wake.
“ Leo tumetembelea Wilaya
ya Mkalama ikiwa ni muendelezo wa siku ya mwanamke Mkurugenzi wetu wa mfuko wa Bima
ya Afya ya Taifa dokta Irene Isaka
ameitoa kwa ajili ya wanawake vifaa vya kujifungulia haya pia ni maono ya Rais
Daktari Samia kwa kina mama,”
Mganga mfawidhi wa Kituo
cha Afya cha Kinyangiri ANNA PETER amesema kuwa vifaa hivyo ni muhimu kwa
wanawake wanapofikia wakati wa kujifunga huku akimpongeza Rais Dokta Samia kwa
jitihada zake kwa wananchi wake.
“ Hivi vifaa vitasaidia
sana kwa wanawake hawa ambao wanaelekea kujifungua lakini pia NHIF nao
tunawashukuru kwa kusambaza vifaa hivi,” DK. ANNA
Kwa Upande wake Dokta
Nikasi Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkalama amesema kuwa vifaa
wamevigawa kwa watu wanaostahili akiwashukuru Bima ya Afya Singida kwa kazi
nzuri wanayoendelea kuzitoa kwani wao kama watoa huduma zitasidia kutoa huduma
bora.
Nao wanufaika wa vifaa
hivyo Ester Samwel na Rechal Misana ambao
ni mama wajawazito wamesema kuwa vifaa hivyo
vitasaidia kupata uzazi salama huku wakishukuru NHIF kwa jitihada zao za
kuzisambaza.
Naye Afisa wa wanachama
NHIF Mkoa wa Singida Tatu Yassin amehimiza wa mama wawakatie bima za afya ili
wasije wakapata taabu wanapofikia wakati wa kujifungua na kuwaomba kujiunga na
NHIF.
“Ni waombe watu wajiunge
na NHIF kwani ni muhimu mno kwa ajili ya maisha yao niwaambie hii ni salama
kwao waje wajiunge wakate bima,” Tatu
Katika msafara huo
wametembelea Kituo cha Afya cha Kinyangiri pamoa na Hospitali ya Halmshauri ya
Mkalama.
Post a Comment