Na Amini Nyaungo
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Jesca Kishoa amewapa tabasamu wanafunzi wa Shule za Sekondari kata ya Nkalakala Wilaya ya Mkalama kwa kuwapa taulo za kile ili waweze kujistiri.Baada ya wanafunzi kupata taulo hizo wakamshukuru Mhe. Kishoa kwa kuwajali, zifuatazo picha zao na maelezo yake.
Picha 1. Wanafunzi wa Shule ha Sekondari Seth Benjamini iliyopo kata ya Nkalakala wakifurahi baada ya kupata taulo za kike kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu Jesca Kishoa aliyoitoa katika ziara yake katika kata ya Nkalakala.Maelezo yao ya walimu hayo hapo chini wakimshukuru Mhe. Jesca Kishoa.
" Uongozi wa shule ya Sekondari Seth Benjamini Kata ya Nkalakala tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kutupatia taulo za kike kwaajili ya wanafunzi na mtungi wa gesi ulio complete,"" Kiukweli hatujawahi Ona kiongozi mwenye moyo wa kujitoa kama wewe,tunashukuru sana na tunakuombea Mungu akuinue zaidi,tunaamini ukipata nafasi kubwa Nkalakala na mkalama kwa ujumla itashine,"
Neno lao la shukrani hilo hapo chini wakishukuru kwa zawadi hizo.
" Shule ya Sekondari Nkinto Wilaya Mkalama, tunatoa shukrani za pekee kwa Mh. Jesca Kishoa kwa kuwapatia wanafunzi wakike taulo za kike kwa ajili ya kujisitiri wawapo katika siku zao, pia kwa adhima hiyo watahudhuria masomo siku zote bila chngamoto yoyote. ## HEDHI SALAMA.!!!,"
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nkinto wakiwa na Mwalimu wao wakipokea taulo za kike kutoka kwa Mhe. Kishoa.
Picha 3. Wanafunzi wa shule ya Sekondari Miganga wakifurahia baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Jesca Kishoa.Maelezo yao baada ya kupokea ni haya hapa chini
" Mzigo umefika Mheshimiwa na wanao wa Miganga wamefurahi"

Post a Comment