Na Amini Nyaungo
WAZAZI wametakiwa kuwafanyia hakika watoto wao ili wawalinde kwa majanga mbalimbali yanayoweza kuzuka katika jamii yoyote duniani.
Hayo ameyasema Sheikh Said Juma Haji Naibu Mudili Chuo cha Nnujum katika hakika ya mtoto Kawaida Hamis Shaban kilichopo Mandewa mkoa wa Singida iliyofanyika Unyinga mkoani Singida.
Sheikh Said amesema kuwa hakika inaweza kumkinga mtoto katika magonjwa ya mlipuko na mifupa yake haivunjika kwa imani ya dini ya Kiislam.
Lakini pia amesema kuwa kwa mujibu wa sheria hakika inafanyika mara tu baada ya mtoto kuzaliwa siku saba za mwanzo au siku 14 na siku 21 kama atashindwa basi anatakiwa amfanyie hakika siku yoyote kabla ya kufikisha miaka 18.
Naye mzazi wa mtoto ndugu Hamis Shaban maarufu kama Muna amesema kuwa ametekeleza jukumu lake kama mzazi katika malezi yake kumfanyia hakika mtoto wake.
" nimetimiza moja ya majukumu yangu kama mzazi hivyo wazazi tuendelee kufuata imani zetu za dini zinavyosema katika utaratibu"Muna
Hakika humfanyia mtoto baada ya kuzaliwa inafanyika katika imani ya Kislam ikiwa mtoto wa kiume anatakiwa Mbuzi wawili ikiwa wa kike anatakiwa Mbuzi mmoja.
Mwisho
No comments: