Amesema kwa kuona jitihada hizo Chama cha Soka Mkoa wa Singida kimeamua kumtunuku cheti.
"Tumempa cheti hiki baada ya kutambua mchango wake Cheif Mgonto katika kuendeleza michezo naomba wadau wengine waige mfano huu," Kitila
Pia amesema kuwa sio wadau wengine hawafanyi hivyo bali hawafuati vigezo na masharti ikiwepo kufika SIREFA kufuata utaratibu wa vibali hivyo ni vyema kufuata utaratibu.
Naye Cheif Mgonto amefurahishwa kwa kutambuliwa na kupata cheti akihahdi kuongeza juhudi katika kuendeleza michezo.
Amesema kuwa anatamani kuona katika ligi yake wachezaji wanaenda mbali zaidi huku akiweka wazi mwakani atainogesha zaidi.
"Nawapongeza SIREFA kwa kuona mchango wangu naahidi kuendeleza ushirikiano na kufanya vizuri zaidi," amesema
Mwisho.
Post a Comment