Na Amini Nyaungo
Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego amewaagiza viongozi mkoani hapa kuwasaidia kina mama,Walemavu na Vijana wanaotaka kupata fursa mbalimbali zinazojitokeza ndani na nje ya mkoa wa Singida hususani mikopo ya asilimia kumi ambayo imeshatoka wapate kwani hayo ndio majukumu yao ya kuwasaidia Wananchi wasipo fanya hivyo mishahara yao itachelewa kutoka.
Dendego amewataka viongozi kusimamia haki pamoja na kuwafikia wananchi vijiji katika kuwapa elimu pamoja na msaada ili waweze kupata mikopo iliyotolewa kwa ajili yao kujikwamua kiuchumi.
Aidha Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng'i Issa amesisitiza kuwa mpango wa asilimia kumi ni muhimu sana, inawasaidia sana wananchi kujiendeleza kiuchumi.
Amesema kuwa Miundombinu ya barabara inapokuwa nzuri biashara itafanyika vizuri huku akiitaja nishati ya umeme ni muhimu katika maisha ya mwanandamu pamoja na Mawasiliano, Ubinafisishaji, kukukuza ujuzi , uzoefu mila , Masoko, ushirika na Uwekezaji.
Mkoa wa Singida Fatuma Mganga ametoa taarifa ya mkoa kwa ujumla wake ikiwemo lishe na hali ya ustahimilivu kwani amesema kuwa mkoa una chakula cha kutosha pamoja na mkakati walionao kuboresha upatikanaji wa chakula pamoja na lishe bora.
Mganga hakuwaacha wanafunzi kwani amesema kuwa Mkoa bado unaendelea kuhamasisha kutoa chakula shule ili wanafunzi wapate kutulia wasome kwa bidii.
Baadhi ya wajasiliamali walioshiriki zoezi hilo akiwemo Edna Malekela amewataka wasimamizi waache mfumo waliotumia zamani wawe wawazi na watoe mikopo kwa kufuata utaratibu uliokuwa bora.
Mwisho
No comments: