Na Amini Nyaungo
MKUU wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amewasisitiza Wananchi wa Mkoani hapa waendelee kujiandikisha katika daftari la kupiga kura wa Serikali za mitaa ambayo imeanza tarehe 11.10.2024.
Ameyasema hayo leo alipokuwa akifanya mahojiano na Standard Radio juu ya umuhimu wa kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na kuwakumbusha utofauti wa uchaguzi huu wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
"Niwaombe Wananchi wa Singida kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mita mimi tayari nimejiandikisha, huu unatofautiana na ule wa mwakani wale waliojiandikisha la daftari la kudumu la mpiga kura wa mwaka 2025 hawezi kupiga kura serikali za mitaaa hivyo aende akajiandikishe hachukui muda mrefu ili apate haki yake ya msingi," Dendego.
Dendego ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha kuwa kupiga kura ni haki ya mwananchi ya msingi hivyo wasikubali kupoteza na njia rahisi kujiandikisha.
"Kupiga kura ni haki ya msingi ya kila mmoja hivyo msikose, mkajiandikishe,"Dendego
Uchaguzi wa Serikali za Mtaa yanafanyika tarehe 27.11.2024.
Mwisho.
No comments: