HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » POLISI MAKAO MAKUU WATOA TAARIFA ZA WALIOUWAWA KWA MGANGA RUVUMA

 

Na Amini Nyaungo 
Jeshi la Polisi makao makuu limetoa taarifa ya wafanyabiashara wawili waliofariki dunia kwa kunywa maji waliyopewa na mganga kisha kulegea na kupoteza maisha mkoani Ruvuma tarehe tatu mwezi huu mwaka 2024.

Taarifa ambayo imetoka Polisi makao makuu inasema kuwa Raymond Hyera maarufu kama Ray mwenye miaka(25), mkazi wa Msamala Manispaa ya Songea na mwenzake Riziki Mohamed mkazi wa mji Mwema mkoani hapo ambapo tukio hilo limetokea Julai 31,2024 na taarifa polisi zimepelekwa Agusti 03,2024.

Taarifa ya polisi baada ya uchunguzi inasema kuwa watu hao walienda kwa mganga anayefahamika kwa jina la Mtila Ausi ambaye aliwahadaa watu hao kwa kuwapa hayo maji yaliyowapelekea umauti na kuwaibia kiasi cha milioni ishirini ambayo walikuja nayo huku wakienda kuwazika katika pori la Mdinguli kijiji cha Mtangashari.

Katika uchunguzi huo wa polisi umebaini ya kuwa wawili hao walipelekwa na mwenza aliyefahamika kwa jina la Amini Phiilfoni Sanga mwenye miaka 26.
Polisi katika kuendelea kuwatafuta watuhumiwa hao walimkamata Amini Phiilfoni huku mganga Mtila Ausi na mwenzake Abdallah baada ya tukio hilo walienda mkoani Dodoma walipopanga chumba kisha kugawana pesa walizozichukua kwa waliowapa maji yaliyowapelekea kufariki, hivyo hadi sasa watu hao watatu wapo mikononi mwa polisi.
Jeshi la Polisi limetoa shukrani kwa wananchi wote ambao wameendelea kutoa taarifa wa kweli na sahihi zinazofanikisha ukamataji wa wahalifu ambao wanafanya vitendo kama hivyo au vinavyofanana na hivyo.

Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply