HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » FEDHA ZA SAMIA ZIMETUMIKA VYEMA SINGIDA, DENDEGO ATHIBITISHA

 Na Amini Nyaungo

Mkoa wa Singida  umepokea kiasi cha shilingi Trilioni 1.9 za fedha kutoka katika serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kutumika katika miradi ya maendeleo kama ilivyoelekezwa.


Hayo ameyasema leo Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego alipokuwa anahutubia katika maonyesho ya 7 ya Uwezeshaji kiuchumi yanayaohusisha mikoa 6 huku Singida ikiwa mwenyeji.
"Tumepokea kiasi cha trilioni 1.9 ambazo tumezielekeza katika mpango wa maendeleo ndani ya mkoa wetu na zimetumika katika miradi ya mendeleo,"Dendego

Dengedo amesema kuwa Rais Samia amaendelea kuitengeneza nchi na katika zoezi hilo Singida imenufaika kupata fedha nyingi ambazo zimetengeneza miundombinu mbalimbali ilikiwemo shule, Hospitali pamoja na kutaka kuukarabati Uwanja wa ndege wa mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akiwa na Waziri wa Nchi William Lukuvi leo wakati wa Maonyesho ya 7 ya Uwezeshaji mkoani Singida.
Amesema siri ya kufanikiwa fedha hizo kuzielekeza katika maendeleo ni pamoja na mshikamano wa viongozi mkoani Singida na kusimamia vyanzo mbalimbali vya mapato.


Maazimisho hayo yameanza tarehe 08.09.2024 na kufunguliwa leo tarehe 10.09.2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Bunge na Uratibu) na itafungwa tarehe 14.09.2024 na Naibi Waziri Mkuu na Waziri ma Nishati Dokta Dotto Bitteko.


Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply