By: Amini Nyaungo
on September 27, 2024
/
Na Amini Nyaungo
Mifuko mia moja ya Sementi imetolewa katika Zahanati ya Isene kata ya Matongo Wilaya ya Iramba mkoani Singida kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Zahanati hiyo kwa ajili ya Wananchi wa eneo hilo.
Mifuko hiyo imetolewa leo na Mbunge wa Viti Maalum Jesca Kishoa baada ya kutoa ahadi ya kuwapatia msaada huo kwa wananchi wake.
"Leo nimekuja na mifuko ya Sementi kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Zahanati hii ambayo itawasaidia wananchi wa maeneo haya na jirani," Kishoa
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Isene Jira Mpanzi amemshukuru Jesca Kishoa kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya pamoja na kuwapigania bungeni kuwepo na kupata huduma za kijamii.
"Tunamshukuru Mheshimiwa Kishoa msaada wake mifuko mia moja ya Sementi anatupigania sana bungeni,"Mpanzi
Wananchi wa Isene wameoneshwa kufurahishwa na utekelezaji wa ahadi ya Kishoa huku wakimuomba aendelee kuwashika mkono.
Zahanati hiyo imeanzishwa mwaka 2017 kwa nguvu za wananchi .
Sambamba na hilo alitembelea zahanati 2 na kugawa mashuka kuwapa mkono wa pole wagonjwa waliolazwa zahanati hapo.
Kwa upande wa vijana na wakina mama, mhe. Kishoa amewashika mkono wamama 6 wajasiliamali wadogo wadogo kwa kuwaongezea mtaji kiasi cha shilingi laki tano (500,000). Pia amegawa mitungi ya gas kwa mama ntilie 30 na jezi za mpira Kwa timu 11 za vijana wa vijiji vyote vitatu vya Kata ya Matongo.
Mwisho.
Tag:
HABARI
CHAMBER MEDIA's Admin
Asante Mfuatiliaji wa Chamber Media Ukiwa na Maoni au Jambo lolote Kuhusu Taarifa Zetu Tafadhali Wasiliana nasi +255 717 519 981 Asante na Endelea Kubaki nasi..
No comments: