Na Amini Nyaungo
Wakazi wa Jimbo la Singida Mashariki mkoani Singida wamenufaika na vifaa vya michezo pamoja na mitaji kwa wajasiliamali kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum kwa Vijana Nusrat Hanje alivyovitoa jana katika Tamasha la michezo lililofanyika shule ya Sekondari Mungaa.
Ametoa vifaa vya michezo katika kata zote ndani ya Tarafa ya Mungaa Jimbo la Singida Mashariki.
"Nimefanya Bonanza la Michezo mbalimbali Tarafa ya MUNGAA jimbo la Singida Mashariki lililohusisha ugawaji wa vifaa vya michezo katika kata za Tarafa ya Mungaa na Ikungi,"Hanje
Hanje amesema kuwa michezo mbalimbali ilifanyika na imekuwa na burudani nyingi micbezo yote ilikuwa na zawadi kwa mshindi wa kwanza na aliyshika nafasi ya pili.
Katika hatua nyingine amewaongezea mitaji vikundi viwili vya kina mama ili waongezee katika harakati zao za kutafuta maisha.
Katika tamasha hilo ambalo limehudhuliwa na watu zaidi ya elfu moja uwanji hapo bingwa ni timu ya Dungunyi FC iliyoichapa Tarafa ya Mungaa kwa mikwaju ya penati.
Mwisho.
No comments: