HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » WANANCHI WATAKIWA KUJUA MAANA YA UKATILI WA KIJINSIA.


Na Sylvester Richard

Wananchi wa Mkoa wa Singida wametakiwa kufahamu maana ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto ili wanapotendewa watoe taarifa na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Hayo yamebainishwa Juni 22, 2024 na Mkaguzi wa Polisi (INSP.) Amina Fakih ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Singida alipokuwa akitoa elimu juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto kupitia kituo cha matangazo cha Standard redio  Singida.

Aidha, Fakih amesema kuwa ukatili wa kijinsia ni hali ya kumnyima haki anayostahili kupata mwanaume au Mwanamke katika jamii ikiwemo haki ya kupata elimu, kumiliki mali, kufanya kazi halali na kuchaguliwa kuwa kiongozi.


Sambamba na hilo, Fakih ameielimisha jamii juu namna ya kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pindi wanapokumbana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ili wachukuliwe hatua na kukomesha vitendo hivyo katika Wilaya na Mkoa wa Singida kwa ujumla.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply