Raymond Jumah, Kenya
Yameongezea kwamba taasisi zote zenye mamlaka kwenye masuala ya usalama ikiwemo idara ya polisi, zafaa kuwatangazia raia, waziwazi, kwamba zinalinda haki ya kila raia kushiriki mikutano ya amani na maandamano ya amani katika siku zijazo.
Baadhi walikumbana na mauti wakati wakijaribu kuingia Bunge la Kitaifa, eneo ambalo Jumanne lilikuwa chini ya ulinzi mkali Mswada tata wa Fedha ukijadiliwa na kufanyiwa marekebisho.
Maandamano yalishuhudiwa maeneo tofauti nchini kupinga kupitishwa kwa Mswada wa Fedha 2024, na idadi ya watu isiyojulikana wanahofiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Mhe. Raila Amolo Odinga ni mojawapo wa viongozi waliokashifu mauaji hayo.
“Ninasikitishwa na ukatili wa polisi kwa vijana waliokuwa wakiandamana kwa amani na kwa mujibu wa sheria… Ninasikitishwa na mauaji, kutiwa nguvuni, kuzuiliwa na msako unaoendeshwa na polisi kwa wavulana na wasichana wetu ambao tu wanataka kusikizwa kuhusu ushuru dhalimu, unaowanyang’anya maisha yao ya leo na ya siku za usoni,” Bwa Raila alisem
Bw Raila, kupitia taarifa rasmi kwa vyombo vya habari alisema "Ni jambo la kusikitisha kuona serikali inatumia asasi zake za kiusalama “kuangamiza watoto ambao waliandamana kwa amani kutekeleza haki yao Kikatiba”.
Mswada wa Fedha 2024 ambao Jumanne mchana ulipitishwa na wabunge, sasa ukisubiri kutiwa saini na Rais Ruto kuwa sheria, unahofiwa huenda ukasababisha maisha kuwa magumu kutokana na ushuru wa ziada (VAT) unaopendekezwa kwa baadhi ya bidhaa na huduma.
No comments: