HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » WANAFUNZI 100 SHULE YA MSINGI MWANDU WANUFAIKA NA MBUNGE KISHOA

Katika kuwajali na kuthamini wananchi Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Singida Jesca Kishoa jana amekabidhi sare (Unifrom)mia moja za wanafunzi wa shule ya msingi Mwandu ambao walikuwa wanauhitaji wa sare hizo pamoja na mtungi wa gesi kwa ajili ya matumizi ya shule hiyo.
Hayo yamefanyika jana Mei 31,2024 kata ya Iguguno Wilaya ya Mkalama mkoani Singida katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na wananchi wa eneo hilo, aidha amesema kuwa taarifa ya juu ya wanafunzi hao kukosa sare za shule aliipata kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo alimwambia namna wanafunzi hao walivyokuwa na uhitaji wa vifaa hivyo na akaona atoe mchango wake kwa kuwapa wanafunzi wapate kuvaa kama waliovyokuwa wengine.
Licha ya hayo ametoa mashuka 100 ya kujifunika wagonjwa katika Zahanati ya Iguguno huku akitoa mafagio  pamoja na Compyuta  ili wahudumu wa zahanati hiyo waweze kuhifadhi mafaili yao vizuri.

Kishoa ametoa mitungi ya gesi kwa mama Ntilie ili kuwaondoa katika matumizi ya kuni.
Ametumia jukwaa hilo kuwapa wananchi nafasi ya kuelezea kero zao ambapo kwa pamoja zililenga katika mahitaji ya wananchi wote wa eneo hilo, ikiwemo, Barabara, Vituo vya afya pamoja na michezo, katika majibu yake amewataka wawe watulivu kwani atachukua maoni yao na kuyapeleka katika Mamlaka husika na yale ya Bungeni atayapigania ili yapate ufumbuzi aidha katika michezo ametoa jezi za timu zote zilizopo katika kata hiyo ikiwa sambamba na mipira.

Kishoa amesema kuwa amefanya hayo yote katika kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply