HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » KISHOA AMPA FARAJA MLEMAVU KWENDA SHULE

 

Faraja imetolewa kwa mlemavu Musa Ramadhani kwa wa Kata ya Iguguno wilaya Mkalama ambaye anachangamoto ya kwenda shuleni kwa kukosa kiti cha kutembelea ambapo Mbunge wa Viti Maalum Jesca Kishoa amempa pamoja kumpatia million moja bibi mlezi wake. 
Kishoa alitoa ahadi hiyo wakati wa kufurahia siku yake ya kuzaliwa ambayo imefanyika Kata ya Iguguno Wilaya ya Mkalama wiki iliyopita.
Baada ya kufanya makabidhiano Jesca Kishoa alimuomba awe mama yake wa hiari kwa upendo wa dhati kwa familia hiyo na mtoto Musa amekubali kwa kububujika na machozi ya furaha.

Siku ambayo alifurahia siku yake ya kuzaliwa alimpa milioni moja bibi mlezi wa mtoto huyo ambapo kiasi hiko cha pesa bibi amenunua kiwanja chenye thamani ya laki saba(700,000) laki tatu zikitumiwa katika kuanza ujenzi wa nyumba hiyo.

Kishoa amewahakikishia kuwa ataendelea kushirikiana nao katika ujenzi waliouanza huku akiendelea kuwasaidia katika mambo mengine.

" Nimefurahi kukutana nanyi leo, tutaendelea kushirikiana katika ujenzi mliounza na mimi nitakuwa mama yako wa hiari," Kishoa.

Kishoa amesema kuwa Musa Ramadhani ambaye ni mlemavu anastahili kusaidiwa ili apate faraja na apate haki yake ya msingi ya elimu kama walivyo watoto wengine.

Kuna kijana Musa anashindwa kwenda shuleni kutokana na changamoto aliyonayo hivyo amemoatia kiti ili aweze kwenda shule na kuungana na wenzake.

Kishoa ameyafanya haya katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa huku  akitatua kero mbalimbali za wananachi kwa kuwapa faraja. 

Mwisho.... 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply