Na Sylvester Richard.
Afisa Maawasiliano wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) upande wa Tanzania Abass Abraham amesema kuwa wananchi wa Tanzania waliopitiwa na mradi huo wameshirikishwa kikamilifu katika kila hatua ikiwemo elimu juu ya uhifadhi wa mazingira, afya, fidia za nyumba na mashamba pamoja na elimu ya matumizi fedha.
Akiongea juu ya fidia kwa watu waliopitiwa na mradi huo, amesema zaidi ya watu 9000 wamepitiwa na mpaka sasa asilimia 99 wamelipwa fidia ya kulipwa fedha au kujengewa nyumba.
Akiongea kuhusu mradi huo ndani ya Mkoa wa Singida Josephat Kanyunyu ambaye ni Mratibu wa Mahusiano wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) Mkoa wa Singida amesema mradi huo umepita Wilaya tatu ambazo ni Iramba, Mkalama na Singida huku watu 1296 wakiguswa na mradi huo.
No comments: