HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » VIJANA MMEJIPANGAJE KUKOPA MWEZI JULAI- NDAHANI

Afisa Maendeleo Vijana wa Mkoa wa Singida Fredricky Ndahani amewauliza vijana wa mkoa wa Singida juu ya namna gani wamejipanga kukopa mikopo nafuu ya asilimia kumi itakayoanza kutolewa kuanzia mwezi wa saba mwaka huu hii imekuja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. Samia Suluhu Hassan kuruhusu kutolewa mikopo hiyo. 

Hayo ameyasema leo ofisini kwake mkoani Singida alipotembelewa na Chamber Media kutaka kujua kauli yake katika maandalizi ya utoaji wa mikopo baada ya tangazo la ruhusa kutoka kwa Rais Samia. 

Ndahani amesema kuwa vijana wanatakiwa wajipange mapema katika vikundi itakapofika wakati wa kukopa iwe rahisi kupatiwa mikopo wakafanye shughuli zao za kujiletea Maendeleo katika familia zao. 
" Vijana wanatakiwa wajipange vizuri wakati huu kabla ya kufika mwezi wa saba ambao ndio mikopo ya asilimia kumi inatolewa, wakijipanga sasa hivi itakuwa rahisi kupata mikopo punde tu itakapoanza," Ndahani.
Aidha amesema ya kuwa mikopo hiyo ilisitishwa ili kuboresha mifumo mizuri ambapo katika mikopo hiyo hakuna riba inayotolewa. 

Mikopo hiyo itatolewa kwa njia ya benki kwa Halmashauri kumi huku sehemu nyingine itatolewa kwa mfumo wa zamani ulioboreshwa. 

Mwisho 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply