HABARI

MICHEZO

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

HABARI

HABARI

MAKALA

» » WAFANYABIASHARA WA MIFUGO EPUKENI MLIPUKO WA TOPE-MACHA

Na Sayi Mathias, Shinyanga



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi  Macha amewataka wafanyabiashara wa mifugo katika mnada wa Mhunze uliopo wilaya ya Kishapu Mkoani humo kuwa makini na kuchukua tahadhari kufuatia mlipuko wa tope  linalolipuka kutoka chini ya aridhi kuja juu katika eneo hilo linalotumika kufanyia biashara hiyo.


Rc Macha ametoa tahadhari hiyo alipotembelea eneo hilo katika muendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayoendelea  wilayani humo ambapo amebaini changamoto hiyo mai 23,2024 na kumtaka  msimamizi wa mradi   unaoendelea  wa ujenzi wa eneo la kuuzia mifugo katika mnada huo  ambaye anatoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi  kuwasiliana na Wataalamu wa miamba ili kuangalia iwapo tatizo hilo haliwezi kuleta madhara katika siku zijazo.


‘’Wala sijaja kuzuia shughuli zisiendelee isipokuwa nimekuja kusema tunapaangalia tuone kama panatufaa kwa keo na kesho,na linguine tumekuja kutoa tahadhari kwasababu kuna mtu alididimia na ng’ombe pia ,hivyo niuombe Uongozi wa soko uzungushie tepe mwekundu maeneo yote yenye tope ili tusije tukapata madhara .’’

     Naye Msimamizi wa mradi wa ujenzi huo Mhandisi  Hamad  Mohamed Abdalah amesema mradi huo ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni 710 umekumbwa na changamoto hiyo ya kulipuka  kwa tope kutoka chini ya aridhi ambapo amehaidi kusimamisha mradi huo kwa muda mpaka pale watakapofika wataalamu wa miamba ili kuainisha endapo eneo hilo liko salama kwa shughuli za kibinadamu.

Nao baadhi ya wananchi waliokuwepo katika eneo hilo wameiomba serikali kushughulikia changamoto hiyo kwa haraka  kwani wamekuwa wakipata  tabu ikiwa ni pamoja na baadhi ya mifugo na binadamu  kuzama na kutitia katika tope hilo,na wengine wakiomba serikali kuhamisha mnada huo na kuupeleka katika maeneo mengine yaliyo salama.



Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply