WANANCHI WAASWA KULIPA KODI KWA WAKATI



Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewaomba wananchi kulipa kodi kwa wakati na kuacha kulimbikiza madeni ili kuepuka kuwa na mzigo mzito wa ulipaji wa kodi. 


Hayo amesema jana na Maafisa wa TRA kutoka makao makuu Dodoma Mercy Macha na Barnabas Masika walipoongea na Standard Radio katika kipindi cha Zinduka wakiomba wasilimbikize madeni walipe kwa wakati. 

Macha ameweka wazi kuwa TRA ni rafiki wa kila mtu ndio maana wanaendelea kutoa elimu ili walipa kodi wasipate shida wakati wa ulipaji, nawashauri walipe kwa wakati ili madeni yasirundikane itakuwa rahisi kwao kufanya baishara zao vizuri.

"Niwaombe walipe kodi kwa wakati ili kuondoa mzigo wa deni kubwa wakati wa ulipaji kwani ukilimbikiza mwisho unakuja kuona deni kubwa,"amesema.

Kwa upande wake Barnabas umeiomba jamii kuacha kukwepa kulipa kodi akieleza kuwa ndio inayoleta maendeleo katika taifa.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post