Baadhi ya wakazi wa Kata ya Ndembezi Halmasahauri ya Manispaa ya Shinyanga wameiomba Serikali kujengea uzio maeneo ya malalo ili kukomesha wizi wa misalaba na vigae katika makaburi yaliyopo Mtaa wa Dome .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa wamekuwa na destuli ya kwenda kufanya usafi makaburini na kukuta baadhi ya misalaba ya iliyoundwa kwa nondo na vyuma imeibiwa na kwenda kuuza kama vyuma chakavu huku vigae vikivunjwa na kuuzwa kwaajili ya matumizi ya jiko na vyoo hali inayosababisha kupotea kwa kumbukumbu ya wapendwa wao .
Kufuatia hali hiyo wameiomba Serikali kuwatafutia mbadara wa kuyajengea fensi na kuwachukulia hatua wanaofanya vitendo hivyo ili kulinda miundombinu iliyopo.
Kwa upande wake Mwenyekiti waMtaa wa Dome Solomon Nalinga amesema Viongozi wa Mtaa huo wameshaanza oparesheni ya kutembelea wafanyabiashara wa vyuma chakavu ili kuwahamasisha kutopokea vyuma chakavu aina ya misalaba ili kukomesha hali hiyo.
Naye Padre Annatory Salawa ambaye ni Paroko wa Palokia ya Mtakatifu Immakulatha Shinyanga Mjini amesema kuwa Jamii haina umakini katika kutunza makaburi hali inayoruhusu vitendo viovu kufanyika katika katika maeneo hayo.
Kaimu Kamanda wa Jeshimla Polisi Mkoa wa Shinyanga Kennedy Mgani amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wanaendelea na upelelezi ili kubaini wanaofanya vitendo hivyo ili sharia ichukue mkondo wake.
Post a Comment