Imeelezwa ya kuwa vijana wasikae nyumbani baada ya kusomeshwa na wazazi wao watumie elimu yao kutoa ujuzi mbalimbali walio nao ili wengine waweze kunufaika na elimu zao.
Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoa wa Singida Ambwene Kajula alipokuwa Standard Radio katika kipindi cha Zinduka kinachoruka Asubuhi akiwataka waliobahatika kupata elimu ya fani mbalimbali watumie elimu yao kuwapa wengine ili wanufaike na kile walichokivuna shuleni.
"Nawaomba watu ambao wamepata elimu wazitumie katika kuleta maendeleo maeneo walipo ili elimu zao ziwe na tija," Kajula
Ametoa mfano Maafisa Kilimo wanaweza kutoa ujuzi wao namna yakilimo bora, ardhi ipi inafaa na kilimo na mazao gani yanapaswa kulimwa ili nawao walime kilimo cha kisasa.
Kajula amesema kuwa katika elimu wanazotoa huko wanapoenda kwa mkoa wa Singida wanajitajidi kuwaeleza vijana wazitumie elimu zao ziwe na manufaa kwa jamii nyingine wakifanya hivyo itaweza kusaidia jamii kujinyanyua kiuchumi.
Aidha hakuacha kuiasa jamii kuacha maswala ya Ukatili wa aina mbalimbali kwani unadhoofisha maendeleo husika ya Taifa Katika maswala ya ukatili ambapo Kajula amesema kuwa inatengeneza chuki na husda kwa familia inayofanyiwa Ukatili.
"Nawaomba ndugu zangu tuache kufanya mambo ya Ukatili kwani yanaondoa utu wa mtu na kutengeneza chuki baina yao," Kajula
Kajula hakuacha kutumia nafasi hiyo kuomba jamii ya mkoa wa Singida kujiunga na familia ya SMAUJATA ili kupinga na kukataza Ukatili wa aina yoyote.
*KATAA UKATILI WEWE NI SHUJAA*
Post a Comment