ARAJIGA PILATO YANGA NA SIMBA , KITILA WA SIREFA NDANI



Bodi ya ligi kuu Tanzania Bara (TPLB) kwa pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wamemteau Ahmed Arajiga kutoka Manyara kuamua pambano la Watani wa Jadi Yanga na Simba litakalofanyika kesho majira ya saa kumi na moja jioni uwanja wa Benjamini Mkapa. 


Huu ni mchezo wa pili baada ya ule wa kwanza Yanga kushinda magoli 5-1, ni mchezo ambao una mambo mengi ndani na nje ya uwanja.

Licha ya Arajiga kuwa maamuzi wa kati Mwenyekiti  wa Chama cha soka mkoa wa Singida Hamis Kitila yeye atakuwa "Match Commissioner" wa mchezo huo. 

Kitila mmoja ya Wenyeviti wa soka vya mikoa wanaofanya vizuri sana hususani mkoa wake wa Singida kila sekta ipo vizuri kuanzia ligi a Wanawake, Vijana hadi katika usimamizi wa Miundombuni. 



Post a Comment

Previous Post Next Post