Baada ya taarifa za mshambuliaji wa Yanga Clement Mzinze kutakiwa na Azam FC kwa dau la miliomi 400 kwa taarifa ya Msemaji wa Wanarambaramba Hasheem Ibwe Sasa nyota huyo anahitajika Watford ya Uingereza.
Taarifa za uhakika tulizozipata Chamber Media ya kuwa Mabosi wa Watford ya Uingereza wamekuja kwa Wakala wa Mzinze Jasmin Razak kuulizia huduma ya nyota huyo.
Watford wamevutiwa na uchezaji wa nyoTa huyo baada ya hivi karivuni kuonyesha uwezo mkubwa.
Lakini pia bado Aza FC nao wamesema wameweka kiasi cha pesa na mshahara mkubwa kumng'oa nyota huyo Yanga kama watakubali ofa yao.
Kwa upande uongozi wa Yanga wapo kimya na wanaendelea na harakati za kuona namna ya kutetea ubingwa ligi kuu Tanzania Bara hivyo hawako tayari kuelezea mambo ambayo hayapo kwa mujibu wa kiongozi ambaye hakutaka kutajwa jina lake
Post a Comment