Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itatoa chanjo ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana kwa mkoa wa Singida inaanzia April 22 hadi 26 mwaka huu katika vituo mbalimbali vya afya ikiwa na lengo la kuwakinga watoto wa kike kupata hatari ya maambukizi ya saratani.
Hayo ameyasema leo Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Singida Jadili Mhanginonya alipoongea na Standard Radio akiutaarifu uma wa mkoa wa Singida wafike katka vituo vya Afya kuanzia tarehe iliyotajwa ili wapate kupata chanjo hiyo.
Chanjo hiyo inatolewa kwa wasichana wnye umri kuanzia miaka 9 hadi 14 kuanzia saa mbili kamili asubuhi.
"Chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi kwa mkoa wa Singida itatolewa kuanzia tarehe 22 hadi 26 mwezi huu niwaombe wazazi wawalete watoto wao wa kike ili wapate chanjo kwa umri ambao nimeutaja," Jadili
Jadili ametumia nafasi hiyo kusema kuwa tangu waanze kutoa chanjo mwaka 2018 kwa mkoa wa Singida wametoa dozi hiyo kwa watu laki moja thelathini na moja mia sita na sabini na saba (131,677).
Ni wanawake Wenye hatari zaidi ya kupata saratani ya mlango wa kizazi ni Wenye wapenzi wengi, waliozaa wakiwa na umri mdogo chini ya miaka 20, wanaovuta sigara
Amesema wanawake Wenye hatari zaidi ya kupata saratani ya mlango wa kizazi ni Wenye wapenzi wengi, waliozaa wakiwa na umri mdogo chini ya miaka 20, wanaovuta sigara
Aidha, dalili za ugonjwa huu ni
Kutokea na Damu ukeni isiyokuwa ya kawaida,
Kupata hedhi isiyofuata UTARATIBU
Kutokea na uteute na majimaji ukeni na wakati mwingine yana harufu mbaya
Maumivu ya nyonga
Maumivu wakati wa kujamiiana

" Kuwa na wapenzi wengi inaweza ikakupelekea kupata saratani ya kizazi, tusiwe na wapenz wengi, wale wanawake wanaaovue sigara wapo katika hatari a kupata saratani ya shingo ya kizazi, "Christoweru
Christoweru amewaasa na kuwaomba Wananchi wa mkoa wa Singida kuwa na utaratibu wa kufika katika vituo vya Afya kuangalia afya zao na wasichana wasidharau hii chanjo inayotolewa na Serikali akiweka wazi kuwa vifo vingi vinatokana na magonjwa yabsaratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.
Mwisho
Post a Comment