IDARA YA MICHEZO SINGIDA YAANDAA MPANGO KAZI

 


Mkuu wa Idara ya Michezo SMAUJATA mkoa wa Singida Elineema Babu amewaomba wazazi mkoani  hapa kuwaruhusu watoto wao walio na vipaji vya kucheza mpira kujaribu bahati yao katika vituo mbalimbali vinavyokuza vipaji vyao. 

Hayo ameyasema leo alipokuwa Mbashara Standard Radio akielezea mipango mbalimbali ya Idara ya michezo huku akitarajia kupata mgeni kutoka Idara ya michezo SMAUJATA Taifa. 

Babu amesema Idara hiyo imejitoa katika kuanzisha ligi ya mpira wa miguu ili kutoa fursa ya kupata vijana mbalimbli wenye vipaji.

Siku ya Jumanne kutakuwa na kikao cha wazazi ,na watu wote wenye vipaji mbalimbali kama vile kuimba,kucheza, na vipaji vingine wote wajitokeze kikao ambacho kitafanyika katika hoteli ya rafiki iliyopo mkoa wa Singida. 

"Tunawaomba wazazi waje siku ya Jumanne tuone namna gani tunaweka sawa jambo hili, "Amesema. 

Post a Comment

Previous Post Next Post