KAMPUNI YA UTENGENEZAJI MELI YA DMG YATAJWA KAMPUNI BORA KATIKA TUZO ZA MOROGORO 2026

 


Na Mwandishi Wetu 



Morogoro, Tanzania – Juni 27, 2026—Kampuni ya Dar es Salaam Merchant Group (DMG) imeendelea kupokea tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa zinazotambua ubora wake katika utengenezaji na ukarabati wa meli nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa na hivyo kuleta chachu ya kusukuma mbele MAENDELEO kwenye eneo la uchumi wa bluu..


Tuzo hiyo yenye heshima kubwa ilikabidhiwa Katika usiku wa tuzo  maalumu za Biashara Morogoro 2026 na Mhe. Adam Kigoma Malima, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, katika hafla ya sherehe iliyofanyika Juni 27, 2026. 


Tukio hilo liliwaleta pamoja wakurugenzi wakuu, wavumbuzi, na maafisa wa serikali kusherehekea mashirika yanayoendesha ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia teknolojia na ubunifu.


Kampuni DMG iliibuka kinara kwa kuwa Kampuni mahili kwenye eneo la teknolojia za utengenezaji meli na mabadiliko kwenye uchumi wa bluu


Ushindi huo wa DMG umekuja wiki chache tu baada ya Kampuni hiyo kutambuliwa na Forbes Africa kama moja ya kampuni chache za daraja la kwanza Katika utengenezaji meli Kwa teknolojia za kisasa barani Afrika.


Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Dar es Salaam Merchant Group Rayton Kwembe alisema heshima hiyo inaakisi miaka ya ubunifu usiokoma na kazi ya pamoja.


“Tuzo hii si ya DMG pekee — ni kwa kila Mtanzania anayeamini kwenye mabadiliko chanya Katika sekta yetu,” alisema Kwembe. 


Kwembe alisisitiza kuwa ushindi huo ni wito wa kufanya zaidi: “Teknolojia ya ujenzi wa meli ni muhimu sana Katika kukuza uchumi wetu hususani kwenye eneo la uchumi wa buluu. Hatuwezi kuleta viwanda bila kuwekeza kwenye technolojia. Tuzo hii imetuletea hamasa kubwa ya kuongeza ununifu kwenye miradi yetu ya ujenzi na ukarabati wa meli nchini."


Kwa upande wake, mgeni rasmi Katika hafla hiyo, Mhe. Adam Kigoma Malima alisifu mchango wa DMG Katika kukuza na kuendelea uchumi wa bluu.



“Kampuni kama Dar es Salaam Merchant Group inathibitisha kuwa Moja ya makampuni ya Kitanzania yanaweza kuongoza Afrika katika teknolojia. Kazi yenu inaendana moja kwa moja na ajenda ya serikali ya kuboresha miundombinu ya biashara na kuvutia uwekezaji wa kimataifa.”


Tuzo za Biashara za Morogoro, sasa zikiwa katika mwaka wake wa 6, hutathmini kampuni kwa ubunifu, uwezo wa kukua, na mchango katika maendeleo ya nchi.


Mfumo wa kiteknolojia wa DMG sasa umesambazwa katika mitambo ya kimkakati na unatazamiwa kupanuka kikanda hadi Afrika Mashariki. Kampuni hiyo pia inaendesha “Chuo cha Teknolojia ya Kimeli” cha mfano kwa ushirikiano na vyuo vikuu vya ndani kujenga ujuzi wa kizalendo.


Wachambuzi wa tasnia na wanauchumi wanasema ushindi huo unaiweka Tanzania kama kitovu kinachochipuka cha ubunifu wa teknolojia za utengenezaji wa meli barani Aftika.


Mshauri mkuu wa teknolojia ya meli, Dkt. Amina Shaban alibainisha kuwa “tuzo ya DMG inaashiria mabadiliko — Afrika Mashariki haitumii tu mifumo ya kimeli ya kigeni, bali inasafirisha suluhisho za kizalendo. Mbinu yao jumuishi kutoka upembuzi yakinifu hadi ukabidhi wa mwisho inaweka alama mpya ya ubora wa viwango katika kanda ya Africa Mashariki.”


Kwa upande wake, Nicholas Gilliard mtaalamu wa uchumi kutoka Mkoani Morogoro alisema: “Kila shilingi inayowekezwa kwenye teknolojia ya kimeli inarudisha mara 3-4 katika thamani ya biashara. Tuzo hii ni utambuzi kwamba DMG inaweza kuendelea kusaidia ukuaji wa uchumi wa buluu wa Tanzania katika kutekeleza Dira ya 2050.


Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post