Breaking News

Trending

{getHabari} $label={recent} $type={Habari3}

WAZIRI MKUU AWAONYA WANAOTAKA KUHARIBU AMANI YA NCHI, ABAINI WANAOLIPWA KUVURUGA AMANI

 Na Amini Nyaungo



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Mwigulu Nchemba amesema kuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa na Katiba, sheria  na miongozo ambapo kila Raia ana haki ya kuifuatilia Katiba ambayo imeweka haki na wajibu hivyo kila raia anatakiwa aifuatilie.



Ameyasema hayo leo Juni,27,2026 katika ziara zake za kikazi Ikungi Mkoani Singida akisema kuwa taifa la Tanzania halistahili kurudi nyuma kama ambavyo ilivyotokea Oktoba 29 huku akibainisha amesema kuwa kuna viashiria vya uvunjifu wa amani wamevibaini baada ya kuwakamata baadhi ya watu wanaotaka kuvunja amani ambao wanalipwa pesa na watu mbalimbali.

Aidha katika hotuba yake amesema kuwa uwepo wa vyama vya siasa vipo kwa sababu ipo Tanzania endapo amani ikichafuka hakutotokea amani ya kuyafanya yote akiongeza kuwa serikali haina ugomvi na vyama vya siasa huku akitanabaisha kuwa kitu kikubwa ni kusimamia amani na usalama wanchi na raia wake.



Waziri Mkuu amesema kuwa kuna watu wanataka kuwatumia vijana waTanzania ili kutimiza ajenda zao za kuichafua Tanzania akisema kuwa kuna baadhi watu wamewakamata ambao wanataka kuwapandikiza ili waichafue nchi.

DKT Nchemba amewahakikishia wananchi wa Tanzania ya kuwa serikali haitowakuwa na mchezo wa watu wa nanmna hiyo wanaotaka kuharibu nchi akisema kuwa sio mtihani wa kwanza kufanyika ambao kutaka kuivuruga nchi.


Waziri Mkuu ameviaguza vyombo vya ulinzi na usalama  kuwa yoyote anayelipwa ili avunje amani wasimchekee.

Mwisho Katika ziara hiyo ilitofanyika Ikungi amesema kuwa kuna watu wanalipwa pesa kila mwezi  ili wawashawishi watu waandamane.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amesema kuwa Mkoa wa Singida upo salama  wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo

Mwisho 

Post a Comment

Previous Post Next Post