WANANCHI WA IPALALYU WAOMBA KUTENGENEZEWA BARABARA


Na Jumbe Ismailly MANYONI       


WANANCHI wa Kijiji cha Ipalalyu,Kata ya Mitundu,wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida wameiomba serikali kupitia Wakala wa barabara za Mijini na Vijijini(TARURA) wilaya ya Manyoni kuwatengenezea barabara ya kutoka Makao makuu ya Kata Mitundu hadi Kijijini hapo ili kuwapunguzia adha wanazopata za kushindwa kusafirisha mazao yao kupeleka kwenye masoko ya kuuzia mazao hayo.

Akizungumza kwenye mkutano wa kusikiliza kero za wafugaji wa Kijiji cha Ipalalyu,Kiongozi wa Wafugaji wa Kijiji hicho,Omari Bakari Makanja akaanza kwa kuzielezea kero za wafugaji na wananchi wa Kipera kwa ujumla.

Aidha Omari aliweka bayana kwamba pamoja na mambo mengine lakini kero mojawapo ni pamoja na ubovu wa barabara ya kutoka katika Kijiji cha Mitundu ambacho ni makao makuu ya Kata hiyo kutokuwa rafiki kwa wananchi wa vitongoji vyote vya Kijiji cha Ipalalyu.

“Kilio cheti kingine mheshimiwa tunaomba barabara zetu kutokea Mitundu hadi hapa Kipera tuboreshewe na kwa kuwa hatuna maeneo ya kutundika mizinga ya nyuki tunaomba tupatiwe maeneo hayo kwani hatutaweza kuharibu misitu kwa kukata miti zaidi ya kutundika mizinga yetu”alisisitiza kiongozi huyo wa wafugaji.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo kutoka Mitundu kwenda Madibira pale majiweni eneo hilo pia barabara zake siyo rafiki kwa kutopitika hivyo tunaomba serikali yetu sikivu ituboreshee.

Neema Msaki ni mkazi wa Kijiji cha Mtakuja alibainisha kwamba licha ya kutokuwa na miundombinu rafiki ya barabara,lakini maeneo ya vitongoji vyetu havina pia huduma za zahanati,hali inayowalazimu kina mama wajawazito kuteseka sana wakati wanapokuwa wakihitaji huduma za kliniki.

“Hatuna huduma ya zahanati hivyo tunahangaika sana mheshimiwa na barabara kutoka Mitundu kuja mpaka kitongoji cha Kisesa,tunahangaika kweli akina mama wajawazito kutoka Kisesa kwenda Mitundu kufuata huduma hizo hivyo tunaomba tupatiwe huduma hizo karibu na makazi yetu”alifafanua Neema kwa niaba ya akina mama wa Kijiji cha Mtakuja

Naye diwani wa Kata ya Mitundu,Utukufu Levu Gwimile alibainisha kwamba pamoja na mahitaji mengine yanayohitajika katika kata ya Mitundu,lakini kwa upande wa wananchi wa Kipera changamoto yao kubwa nyingine ni miundombinu ya barabara kuwa mbovu na kuna maeneo yaliyokatika kabisa na kufanya kutopitika kwa urahisi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni,Jumanne Ismaili Makhanda akampongeza Mbunge wa jimbo la Itigi,Yohana Stephen Msita kwa jitihada zake za kuwawakilisha wananchi waliomchangua kwenye  vyombo vya maamuzi kupitia kwenye vikao halali

Mbunge wa jimbo la Itigi,Yohana Stephen Msita aliweka bayana kwamba kutokana na neema ya mvua kubwa zilizonyesha zimesababisha miundombinu ya barabara kutopitika.

“Mie barabara zote hizi nazijua kwa sababu nimepita mpaka kule Isanja,kwenda Makuga kote nimepita,ilifika mahali gari likashindwa kupita nikamwambia dereva rudi nikapanda pikipiki na nilifika maeneo Fulani nilazimika kutembea mpaka wa miguu,mimi ni mtoto wa mkulima hata kutembea kwa miguu sioni shida,lakini barabara zetu zina changamoto kubwa sana”alisisitiza Msita

MWISHO.

Post a Comment

Previous Post Next Post