WAFANYAKAZI WA MAHAKAMA SIJGIDANWATAKIWA USHIRIKIANO

 Na Amini Nyaungo



Watumishi wa Mahakama kuu Masijala Ndogo Mkoa wa Singida wametakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kuwasaidia Wananchi katika kuwahudumia kesi zao ili zifanyike kwa haki na weledi.


Hayo ameyasema Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masijala ndogo Mkoa wa Singida Ayoub Yusuph Mwenda alipokuwa anaongea na watumishi wa mahakama Mkoa wa Singida.


"Naomba tushirikiane kwa kila jambo tukiwa na ushirikiano kila sehemu tutakuwa sawa," Jaji Ayoub Mwenda


Aidha katika hatua nyingine Ayoub Yusuph Mwenda- Jaji Mfawadhi Mahakama Kuu Masijala Ndogo Singida amewataka kuwa na nidhamu pindi wanapotoa huduma.


"Nidhamu ni muhimu sana naamini ushirikiano wa kila mmoja ili tuweze kufanikisha na kazi yrtu iwe rahisi," Ayoub Mwenda -Jaji Mfawadhi Mahakama Kuu Masijala Ndogo Singida



Akisoma taarifa ya Afisa Utumishi wa Mahakama ya Mkoa wa Singida Eva Leshange- Afisa Utumishi wa Mahakama Mkoa wa Singida amesema kuwa malalamiko yamepungua kutokana na utoaji wa elimu.


Mahahama hii imeanza kazi rasmi siku ya leo march 30,2026 ambapo sasa kesi zote ambazo zilitakiwa kwenda Dodoma zitashghulikiwa Mkoani Singida.

Mwisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post