WANANCHI WAAMBIWA KUTUMIA VIPIMO KUUZA BIDHAA

 

Na Amini Nyaungo



Wananchi wametakiwa kuwa na desturi ya kutumia mizani katika biashara ili haki itendeke kwa wanunuzi wa bidhaa zao.


Hayo ameyasema wakala wa vipimo Mkoa wa Singida Wille Amos alipokuwa anaongea na Standard Radio juu ya matumizi sahihi ya mizani.


Amos amesema kuwa unapotumia mizani kuna uwezekano mkubwa unaye nunua bidhaa yoyote ikawa katikaa ujazo uliosahihi na unaohitajika.

Katika wakati mwingine amewaomba wauzaji nyanya, Vitunguu na bidahaa nyingine pia watumie mizani ili iendenane na biashara nyingine.


"Hata katika vitunguu au nyamya kote inatakiwa wawe wanapima kupitia vipimo ili mteja apate kunufaika na haki," Amos


Aidha ametumua jukwaa hilo kuwaomba wafanyabiashara kuanza kutumia mizani wakati huu kabla hawajaanza kutumia sheria kali.


Amos amewaomba pia wanaonunua bidahaa wawe makini kuangalia namna wanavyopimiwa bidhaa zao kwani wafanyabiashara wengine hawana uaminifu.

Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post