Na Charles Kikoricho
Katibu tawala Mkoa Singida Dkt Fatuma Mganga amewaomba wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi wakati akifungua mafunzo ya uwezaji wa wanawake kiuchumi na kushiriki katika Uongozi.
Dkt Mganga amesema hayo leo November 18/2025 katika ukumbi wa ofisi ya ukaguzi Manispaa ya Singida wakati akizungumza na wawakilishi wa wanawake makundi mbalimbali ambao wanatekeleza afua mbalimbali za usawa wa kijinsia.
Katika ufunguzi wa mafunzo hayo Dkt Mganga amesema ili wanawake aweze kushiriki vizuri katika kugombea nafasi mbalimbali ni lazima waweze kujiboresha katika eneo la kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji kama vile uvugaji wa kuku, kuwa na matumizi bora ya pesa pamoja na kutambua kero ambazo zinawakabili wananchi.
Awali katika ufunguzi wa mafunzo hayo afisa maendeleo kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Irene Beichumila amewaomba wawakilishi wa makundi ya wanawake watakaopata mafunzo haya ya wanawake na uongozi waende kuwa mabalozi wazuri kwa kufikisha elimu waliyoipata kwa wanawake wengine katika Jamii.
Mwisho.




Post a Comment