MASSAWE ATAANZA NA MIUNDOMBINU MISUNA

Na Amini Nyaungo



Mgombea Udiwani wa Kata ya Misuna Manispaa ya Singida Fulgenzi Massawe amesema kuwa kama atachaguliwa kuwa Diwani wa Kata hiyo atahakikisha kuwa Miundombunu ya Barabara ataifanya kuwa kipaumbele chake namba moja katika Kata hiyo.



Hii amesema baada ya kuchukua fomu ya uteuzi kiwania nafasi hiyo ya Udiwani kata ya Misuna.



Aidha ameongeza kuwa kipaumbele chake kingine ni  elimu kupitia shule za Kata ataimarisha shule hizo ziweze kufaulisha wanafunzi wengi.



"Kata ya Misuna ina changamoto kubwa katika Miindombinu, kilio chetu juu ya shule zetu za Kata ili zifaulishe vizuri kupitia shule hizi," 



"Kama mgombea naahidi kwenu naenda kutumika muda wowote ili Kata yetu iwe kioo ya kata nyingine zote," Ameongeza

Post a Comment

Previous Post Next Post