GWAU, MATTEMBE WAPETA VITI MAALUM SINGIDA

 

Na Amini Nyaungo

MAELEZO: MARTHA GWAU ALIPOKUWA MANYONI AKIWA NA UWT AKITOA MAFUNZO MBALIMBALI 

Mkoa wa Singida umewarudisha Martha Nehemia Gwau  pamoja na Aysharose Mattembe kuwania ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kama ilivyokuwa uchaguzi uliopita.

MAELEZO: HAPA MARTHA GWAU ALIKUWA IRAMBA ALIPOKUWA KATIKA ZIARA ZAKE

Martha Gwau ameibuka nafasi ya kwanza katika kura za wajumbe baada ya kukusanya kura 922 kati ya kura 1072 walizopiga wajumbe. Wakati huo Aysharose Matembe amepata kura 676 kati ya 1072.



Kwa upande wa Martha Gwau imedhihirika dhahiri utendaji kazi wake mzuri ndio ambao umempa kura nyingi pamoja na imani ambayo waliyokuwa nayo wajumbe wa Umoja wa wanawake Mkoa wa Singida.


Mhe. GWAU alijitahidi kushiriki katika mambo mbalimbali ya kijamii na chama ikiwa ni msingi wa utu na utulivu pamoja na uzalendo wake kama ambavyo dhamira yake  alivyoomba kuwa Mbunge wa kiti hicho.



Baada ya tukio hilo Gwau amewashukuru wajumbe na kuahidi kufanyakazi zaidi ya alivyofanya nyuma.


"Niahidi kufanyakazi kwa karibu na  nitashirikiana nanyi vizuri kabisa na kazi itaendelea vizuri,"



Mhe. Gwau alishirikiana vizuri katika kipindi kilichopita kupitia shughuli mbalimbali za chama, Umoja wa wanawake na kuviwezesha  vikundi mbalimbali vya vijana.


Mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post